Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi ( CUF), Prof. IBRAHIMU LIPUMBA, amekanusha taarifa kuwa alikuwa mahututi wakati akipelekwa nchini INDIA alikokwenda kupatiwa matibabu baada ya kubainika kuwepo kwa makovu kwenye bandama.
Prof. LIPUMBA amesema alikwenda nchini humo kwajili ya matibabu ya kawaida na kwamba kwa sasa hali yake inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji na kupewa dawa huku akitakiwa kupumzika kwa mwezi mmoja kabla ya kuendelea na majukumu yake.
Kuhusiana na tatizo la mgao wa umeme unaoendelea nchini Prof. LIPUMBA amemtuhumu Waziri WILLIAM NGELEJA kwamba sio muwazi na amekuwa haelezi ukweli kuhusiana na ufinyu wa bomba la SONGAS linalosambaza gesi kwenye mitambo ya umeme.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi CUF Prof. IBRAHIM LIPUMBA amerudi nchini kutokea India alikoenda kupatiwa matibabu ambapo amefanyiwa upasuaji ili kutibu makovu yaliyokuwa kwenye bandama na kubainisha kwamba kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na atapumzika kwa mwezi mmoja kabla ya kuendelea na kazi zake.
Kuhusiana na tatizo la mgao wa umeme unaoendelea nchini Mheshimiwa LIPUMBA amemtuhumu Waziri WILLIAM NGELEJA kwamba sio muwazi na amekuwa haelezi ukweli kuhusiana na ufinyu wa bomba la SONGAS linalosambaza gesi kwenye mitambo ya umeme.
Katika hatua nyingine amezungumzia hatua ya aliyekuwa Mbunge wa Igunga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ROSTAM AZIZ kujivua nyadhifa zake zote ndani ya chama hicho ikiwemo Ubunge.
No comments:
Post a Comment