Monday, July 18, 2011

WAZIRI MAIGE AZINDUA MRADI WA VODACOM FOUNDATION SERENGETI WILD DOGS CONSERVATION PROJECT!

Waziri wa wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige akijadiliana kuhusiana na masuala ya uhifadhi na utalii na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Dietlof Mare,kabla ya uzinduzi rasmi wa mradi wa (Vodacom Foundation Serengeti Wild Dogs Conservation Project) Kulia ni mjumbe wa bodi ya wadhamini ya Vodafone Foundation toka nchini Uingereza, Bi Elizabeth Filkin.

Na Mwandishi wetu, Serengeti.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, juzi amezindua mradi wa uhifadhi Mbwa Mwitu ujulikanao kama “Vodacom Foundation Serengeti Wild Dogs Conservation Project” katika hifadhi ya taifa ya Serengeti, mradi ambao unafadhiliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kiasi cha dola zakimarekani 450,000 kwa miaka mitatu.


Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi huo , Waziri Maige alisema Mbwa mwitu ni miongoni mwa wanyamapori ambao wapo hatarini kutoweka duniani hivyo jitihada kubwa zinahitajika kuwalinda na kuwahifadhi.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akimkabidhi sanamu ya mbwa mwitu Mkurugenzi wa shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA Allan Kijazi kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wa utunzwaji wa mbwa mwitu katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti (Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs Conservation Project). Mradi huo ulizinduliwa juzi na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige (katikati) ambapo Vodacom Foundation imetoa dola za Kimarekani 450,000 kwa miaka mitatu.

Waziri Maige alisema katika bara la Afrika kuna idadi ya Mbwamwitu, wanaofikia 8000 na Tanzania pekee ina jumla ya mbwamwitu 3500 ambao wapo hatarini kutoweka hivi sasa. Alisema katika hifadhi ya Serengeti makundi ya Mbwamitu ambayo yalikuwa yanaonekana sasa yametoweka na mara ya mwisho mbwamwitu wawili tu walionekana mwaka 1998. Waziri Maige alisema, Mwa mwitu hao, wamekuwa wakitoweka kutokana na kuuwa na wananchi baada ya kula mifugo yao , kuugua magonjwa mbali mbali ikiwepo kichaa cha mbwa.


“Napenda kuwapongeza Vodacom kwa kujitokeza kudhamini uhifadhi wa mbwamwitu kwani wanasaidia kuvutia watalii kuja Tanzania na hivyo kuongeza pato la taifa”alisema Maige.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare, wakifurahia jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, baada ya kuwasili kwenye kambi ya utalii ya Soroi, Serengeti kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa kuhifadhi mbwa mwitu (Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs Conservation Project) katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Alisema sekta ya utalii nchini inachangia asilimia 17 ya pato la taifa hivyo ni wajibu wa makampuni kusaidia sekta hii kwani imeajiri zaidi ya watu 700,000 ambao pia ni wateja wa kampuni mbali mbali.


Awali Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania Dietlof Mare..alisema kampuni hiyo, imeamua kujitokeza na kusaidia sekta ya utalii ili kuongeza pato la taifa. Alisema Vodacom inaamini kuwa Tanzania ni nchi ya kipekee duniani katika sekta ya utalii kutokana na kuwa na vivutio vingi na hivyo lazima vitunze na kuhifadhiwa.


“Vodacom tumeamua kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano kusaidia sekta ya utalii na tunaamini katika ufadhili wetu, mbwamwitu waliohatarini kutoweka sasa watarejea hifadhi ya Serengeti”alisema Mare.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare(kulia)akimuonyesha kitu Afisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bi Mwamvita Makamba kwenye kambi ya utalii ya Soroi, Serengeti wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuhifadhi mbwa mwitu (Vodacom Foundation’s Serengeti Wild Dogs Conservation Project) katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori,(TAWIRI) Dk.Simon Mduma alisema TAWIRI ambao ndio wasimamizi wa mradi huo watahakikisha wanashirikisha jamii kuwalinda na kuwahifadhi Mbwa mwitu.
Mduma alisema katika siku za karibu makundi ya Mbwamwitu yamekuwa yakionekana katika pori tengefu la Lolindo na vijiji vya Tarafa ya sale ikiwepo Samunge na tayari umewekwa utaratibu wa kuwafuatilia na kuwalinda.

No comments:

Post a Comment