Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamejitokeza kwenye banda la Wizara ya Maliasili na Utalii lililopo kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere ‘Sabasaba’ kuhudhuria maonesho ya wiki moja yaliyoandaliwa na Wizara hiyo.
Msemaji Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, GEORGE MATIKO, amesema lengo la maonyesho hayo ni kuonyesha mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Wizara hiyo katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.
Naye Afisa Wanyamapori Mkuu wa Wizara hiyo, TWAHA TWAIBU, amemwelezea Mnyama aina ya Sokwe mwenye tabia kama za binadamu kuwa anapofugwa anauwezo wa kuishi miaka 60 huku akiwa na uwezo wa kuzaa mtoto mmoja na kubeba mimba kwa muda wa miezi 8.
Aidha Wizara ya Maliasili na Utalii mapema hii leo inatarajia kuzindua Wakala wa huduma za Misitu katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment