Tuesday, July 5, 2011

MAKAMU WA RAIS USO KWA USO NA MAALIM SEIF SABASABA BAADA YA KUZINDUA GS 1!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati walipokutana kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere katika Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa leo Julai 04, 2011.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DKt. Mohammed Gharib Biala, akisikiliza maelezo ya mjasiliamali, Angela John, kuhusu mashine ya Kusokota, wakati alipotembelea katika Banda la Sido kwenye Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Power Electronics & Controls Ltd, Kayungi Kayungi, kuhusu Mashine ndogo inayozalisha Umeme kwa kutumia maji, wakati alipotembelea Banda la Sido kwenye Maonyesho ya 35 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment