Wednesday, July 20, 2011

WAKAZI WA MANISPAA YA TEMEKE WAHARIBU MAJENGO YA SHULE YA MSINGI SERENGETI!

Wakazi wa Manispaa ya Temeke, Jijini Dar es salaam, Wanadaiwa kuharibu baadhi ya mali za shule ya msingi Serengeti iliyoko katika Manispaa hiyo Wakipinga hatua ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa mengine katika kiwanja cha Shule hiyo.

Akizungumzia hali hiyo, Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Temeke, JOYCE MSUMBA, amebainisha kuwa baadhi ya mali zilizoharibiwa na Wakazi hao ambao wengi wao ni vijana ni pamoja na tofari 400, kwa madai kuwa endapo eneo hilo litajengwa watakosa eneo la michezo sambamba na eneo la kufanyia shughuli mbalimbali za kijamii.

Aidha Bi MSUMBA ameongeza kuwa vijana hao wamejiwekea utaratibu wa kushinda eneo la kiwanja cha shule kwa lengo la kulinda lisitumiwe na watu wengine ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa Shule ya Serengeti.

No comments:

Post a Comment