Wednesday, June 15, 2011

VODACOM YACHANGIA MILIONI 40/- HOSPITALI YA CCBRT!

Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans kushoto ,Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba wakisaini makubaliano ya Vodacom Foundation kuchangia shilingi Milioni 40 za ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto kwenye Hospitali mpya ya CCBRT Boabab itakayojengwa jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia katikati Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule na kulia Meneja Mahusiano wa CCBRT Kira Thomas.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT Erwin Telemans kushoto akipokea kutoka kwa Afisa Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba mkataba wa Vodacom kuchangia shilingi milioni arobaini katika ujenzi wa wodi ya wanawake na watoto kwenye hospitali maalum ya wanawake ya CCBRT Boabab itakayojengwa jijini Dar es salaam.Kulia ni Meneja Mahusiano wa CCBRT Kira Thomas.

Na Mwandishi Wetu

Dar es salaam 14 June, 2011. Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom,kupitia kitengo chake cha kusaidia jamii cha Vodacom Foundation imekabadhi shilingi milioni arobaini kwa taasisi ya CCBRT kuchangia ujenzi wa hospitali ya Baobab ambayo itakuwa ni maalum kwa huduma za afya za wanawake na watoto.

Mkataba wa makabidhiano umetiwa saini jijini Dare s salaam kati ya Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Mwamvita Makamba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Erwin Teleman ambapo wote kwa pamoja wamezungumzia mradi huo wa ujenzi wa hospitali na matumani ya siku za baadae katika kusaidia wanawake na watoto.

Akizungumza katika hafla hiyo Mwamvita amesema suala la Tanzania kuendelea kuwepo katika orodha ya nchi kumi zinazoongoza kwa vifo vya akina mama linapaswa kupiganiwa kwa pamoja na wadau wote ili kunusuru maisha ya wanawake na wataoto.

Amesema Vodacom ni kampuni inayoguswa na ustawi wa maisha ya watanzania na ni imani ya kampuni hiyo kwamba ujenzi huo utawagusa wadau wengine na kuchangia kukamilisha lengo huku akiipongeza CCBRT kwa mchango wake wa kusaidia upatikanaji rahisi na wa gharama nafuu wa huduma za afya hususan kwa makundi yenye uhitaji maalum.

“Kwa kweli inauma sana kuona wanawake wa kitanzania wakipata shida ya huduma za afya serikali imekuwa ikichukua juhudia mbalimbali kukabiliana na changamoto hii pamoja na taasisi za afya kama CCBRT zote hizo hazina budi kuungwa mkono na kuongezewa nguvu ili taifa liweze kukabiliana kwa ukamilifu na changamoto hiyo”Alisema Mwamvita.

Amesema Vodacom itaendelea kuisaidia CCBRT katika azma yake ya kutoa huduma bora na rahisi kwa jamii za watazania katika nyanja ya huduma za afya huku akitoa wito kwa wadau wengine kujiotokeza na kuchangia mradi huo wa ujenzi wa hospitali.

“Leo tunakabidhi shilingi milioni arobaini ambazo ni ahadi tuliyoitoa kuitikia wito wa Rais Jakaya Kikwete wakati alipoongoza harambee ya kuchangia fedha za mradi huu wa hospitali ya wanawake na watoto lakini Vodacom haitoishia hapa tutaendelea kuwa karibu na nyie na kuwahamaisha pia marafiki zetu nao kuwaunga mkono ili lengo litimie”Aliongeza Mwamvita.

Mwamvita amesema afya ni miongoni mwa vipaumbele vya kampuni ya Vodacom katika kusaidia jamii na ndio maana eneo la afya hutengewa zaidi ya asilimia arobaini ya bajeti kwa mwaka zinazotumika kujenga wodi na ukarabati wa miundombinu ya hospitali na vituo vya afya vijijini.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT Erwin Teleman amesema mradi huo ni wa ubia kati ya serikali na CCBRT na kwamba unalenga kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga wanaozaliwa vinavyosababishwa na changamoto za afya ya uzazi nchini.

“Haifurahishi kuona wanwake wakirudishwa vijijini wakiwa kwenye maejeneza kwa sababu ya huduma za afya hasa za uzazi hili halivumiliki na tunataka kuona wanawake wakifurahia maisha serikali imetupatia ardhi na kuahidi vifaa tiba CCBRT inasimamia ujenzi na baadae menejementi ya hospitali pamoja na utoaji wa huduma, alisema Teleman.

Amesema ujenzi unatarajiwa kuanza wakati wowote kwa kuwa kazi ya ubinfu na michoro imeshakamilika huku akisishukuru Vodacom kwa kkuwaunga mkono katika mradi huo.

No comments:

Post a Comment