Wednesday, June 15, 2011

OIKO CREDIT KUKOPESHA ZAIDI YA BILIONI 15 KUFIKIA MWISHO WA MWAKA HUU!

Watanzania wametakiwa kuchangamkia fusra ya mikopo iliyopo, ili wananchi wapatao laki moja na elfu ishirini wawezeshwe kukopa zaidi ya bilioni kumi na tano zilizotengwa, mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Meneja wa Shirika lisilo la kiserikali linalowawezesha watu wenye uhitaji la OIKO CREDIT, Bw DEUS MANYENYE amesema mbali na kuiwezesha miradi ya bilioni 26 toka walipoanza mwaka 2006 hapa nchini, wana mpango wa kupanuka zaidi ili kukamilisha miradi kumi na nne waliyojiwekea kwa mwaka huu.
Aidha amesema miradi yenye thamani ya bilioni 4.5 iko mbioni pia kupitishwa, kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii, kilimo, mashuleni na katika SACCOS.
Mkutano huo mkuu wa Oiko credit hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kutathmini maendeleo na changamoto zinazowakabili, na kwa mwaka huu mkutano huo mbali ya kushirikisha wawekezaji wa nchi tofauti duniani, umemshirikisha Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye aliwakilishwa na naibu wake Bw Mahadhi J. Maalim.

No comments:

Post a Comment