Tuesday, May 10, 2011

UVCCM KUFANYA UCHAGUZI KUZIBA PENGO LA HAMAD MASAUNI!

                                                   MFAUME KIZIGO (Kushoto)
Umoja wa Vijana wa CCM, unatarajia kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Umoja huo kati ya August na Septemba Mwaka huu, Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja huo, BWANA HAMAD MASAUNI.

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, MFAUME KIZIGO, amesema nafasi hiyo inatarajiwa kujazwa na Mwanachama wa Chama hicho kutoka Tanzania Visiwani kufuatia Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo wa sasa, BWANA BENO MALISA kutokea Tanzania Bara.
Aidha ameongeza kuwa Umoja huo umeamua kujaza nafasi hiyo ambayo inajazwa baada ya Uchaguzi wa Kikanuni uliofanyika Desemba, 2008, kufuatia Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwaamuru kujaza nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment