Tuesday, May 10, 2011

MANISPAA YA ILALA KUFANYA TATHMINI YA MABANDA YALIYOUNGUA SOKO LA MCHIKICHINI!

                                     Meya wa Manispaa ya Ilala, JERRY SLAA

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imepanga kufanya tathmini ya uharibifu wa mali uliotokea baada ya mabanda zaidi ya 60 ya kitengo cha mafundi cherehani kuteketea kwa moto katika soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na kituo hiki, Meya wa Manispaa ya hiyo JERRY SLAA amesema kukamilika kwa tathmini hiyo kutawawezesha watendaji wa Manispaa yake kuangalia namna ya kuwasaidia wafanyabiashara walioathirika ikiwemo suala la kufidia mali zao.
Hadi sasa chanzo cha moto huo unaosadikika kuchangiwa na pasi ya mkaa iliyosahaulika katika moja ya banda ndani ya soko hilo bado haijathibitishwa.

No comments:

Post a Comment