Friday, March 16, 2012

SIKU SBL ALIPOKABIDHI HUNDI YA MILIONI 10.9 KWA JUKWAA LA WAHARIRI TEF IKIWA NI TUZO KWA HABARI ZA UTAWALA BORA!

Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL, Bi Teddy Mapunda akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi mil 10,925,000/= kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) (kulia) Bw.Absalom Kibanda na MKurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Bw.Kajubi Mukajanga,hundi hiyo imetolewa leo kwenye hafla ya tuzo za EJAT fupi ya kukabidhi ikiwa ni sehemu ya udhamini wa tuzo ya uandishi wa habari katika masuala la Utawala Bora (Good Governance Category),Kushoto ni Meneja Miradi wa SBL,Bi Nandi Mwiyombela.

Pichani kati ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa SBL ,Bi Teddy Mapunda akizungumza leo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi kwa ajili ya tuzo za EJAT,jijini Dar es Salaam."kwa mantiki hiyo,tukiwa kama wadau katika tasnia hii ya habari,tutadhamini tuzo ya uandishi wa habari katika masuala ya Utawala Bora ( Good Governance Category) kwa kiasi cha shilingi mil 10,925,000/=,Wajibu wetu katika kusaidia shughuli zinazolenga kuboresha tasnia ya habari ni moja ya malengo yetu makubwa.


Mwaka jana tumeweza kutumia zaidi ya shilingi milioni 100 kufanikisha shughuli za chama chama cha waandishi wa michezo Tanzania (TASWA) ambao pia ni wadau wa MCT"alisema Bi Teddy Mapunda.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw.Absalom Kibanda na shoto ni MKurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT),Bw.Kajubi Mukajanga.

No comments:

Post a Comment