Thursday, March 8, 2012

GEITA, KATAVI,NJOMBE NA SIMIYU SASA YATAMBULIWA RASMI KUWA MIKOA YA TANZANIA BARA!

Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema SERIKALI imetangaza rasmi mikoa mipya minne ambayo ni GEITA, KATAVI, NJOMBE NA SIMIYU na wilaya mpya 19 ambayo imechapishwa katika Tangazo la Serikali Na. 72 na kutiwa saini na Rais JAKAYA KIKWETE.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari kutoka ofisi ya Waziri Mkuu imeeleza kuwa makao makuu ya mikoa hiyo mipya yatakuwa Geita kwa mkoa wa Geita, Simiyu yatakuwa Bariadi, Njombe yatakuwa Njombe na Katavi makao makuu yake yatakuwa Mpanda.


Kutangazwa rasmi kwa mikoa hiyo kumekuja baada ya Rais Kikwete kutangaza uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya 21 Julai 2010, kabla hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge. Hata hivyo, baada ya kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa maelezo ya mipaka hiyo vizuri, wilaya zilipunguzwa na kubakia 19.

No comments:

Post a Comment