Thursday, March 8, 2012

WANAFUNZI WALIOSIMAMISHWA NDANDA WAREJESHWA SHULENI!

Hayati Baba wa Taifa Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE enzi za uhai wake aliwahi kunukuliwa akisema amani na utulivu ndani ya taifa lenye Serikali makini, vitapatikana endapo tu serikali hiyo haitajiingiza katika migogoro na wananchi ama taasisi zake.



Kwa kutambua busara hizo hii leo Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi imetangaza kuwarejesha masomoni wanafunzi 61 wa kiislamu kutoka Shule ya sekondari Ndanda iliyopo Mkoani Mtwara,ambao walisimamishwa masomo mwanzoni mwa mwezi januari mwaka huu kwa kile kilichodaiwa ni kuvunja sheria na taratibu stahiki za shule hiyo.


Naibu waziri wa wizara hiyo SELESTINE GESIMBA amesema maamuzi hayo yametokana na makubalino baina ya wizara na jumuiya ya wanafunzi wa kiislamu nchini TAMSYA.


Kwa upande wake Rais wa jumuiya wanafunzi wa kiislamu nchini JAPHARI MNEKE amesema wameridhia maamuzi waliyoafikiana na wizara,huku akitangaza rasmi kusitisha maandano yaliyopangwa kufanyika nchini nzima kuanzia march 9 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment