Thursday, March 8, 2012

MGOMO TAZARA WAISHA, TRENI YA ABIRIA YAANZA KUTOA HUDUMA TENA KUELEKEA KAPIR MPOSHI ZAMBIA!

Hatimaye serikali imeamua kuingilia kati mgomo wa Wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), ambao umechukua takribani siku mbili.

Katika kulinusuru Shirika hilo dhidi ya mgomo huo Waziri wa Uchukuzi OMARI NUNDU, amekutana na Wafanyakazi hao na kuahidi kuyafanyia kazi madai yao yote hatua iliyowafanya warejee kazini na kuendelea kutoa huduma ya usafiri huo.


Akizungumza na kituo hiki, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli nchini (TRAWU), Bwana ERASTO KIWELE amesema kuwa wamefikia hatua hiyo mara baada ya Serikali kuahidi kutekeleza madai yao ikiwa ni pamoja na kuwaingizia mishahara Wafanyakazi wote wa TAZARA kwenye akaunti zao ifikapo marchi 15 mwaka huu.


No comments:

Post a Comment