Monday, December 19, 2011

NDOVU SPECIAL MALT YAWAALIKA WATEJA KWENYE KAMPENI YA 'KUTAZAMA KWA UMAKINI'!


Ndovu Special Malt imezindua kampeni mpya ‘ANGALIA KWA MAKINI’ na kuwaalika wateja wake “kuangalia kwa makini” kile ambacho kinaipa Bia ya Ndovu ladha nzuri na ya kipekee, na kuifanya iwe bia bora zaidi yenye kiwango cha kimataifa.


Ndovu Special Malt imekuwa chaguo la wanywaji wengi wa bia nchini Tanzania ikiwa ni bia pekee ya kitanzania yenye hadhiya kimataifa.


Ndovu ilithibitishwa kuwa na kiwango cha kimataifa pale iliposhinda tuzo ya juu ya Grande Gold katika tuzo za Monde Grande Selection mwaka 2010. Tuzo hizi za “Grand Gold” hutolewa kwa bia zenye viwango vya ubora unaoazia asilimia 90 mpaka 100. Mpaka sasa tuzo hii imetolewa kwa Bia ya Ndovu pekee.
PAMELA KIKULI ambaye ni Meneja Bidhaa Ndovu Special Malt (Kulia) akionesha bia aina ya ndovu kama ishara ya kuzindua kampeni ya Kutazama kwa Umakini yenye lengo la kuwaonesha kimea angavu, Crystal Malt ambavu ambacho hakipatikani ndani ya bia nyingine hapa nchini. Kushoto ni GAUDENCE MKOLWE ambaye ni Mpishi Mkuu TBL.

Imebainika kuwa kuongezeka kwa ubunifu kunakofanywa na wataalamu wa ndani ya nchi, kumechangia ongezeko la matumizi ya zao la shairi na ulezi, hivyo kuwahamasisha wakulima kulima mazao hayo kibiashara.

Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Angalia kwa Makini, meneja bidhaa wa bia ya ndovu Bi. Pamela Kikuli, amesema kuwa lengo la kampuni ya bia nchini TBL, ni kuwaona wateja wao wakitumia bidhaa zinazojali afya zao.


Ni nini kinachofanya Ndovu iwe Bia ya kipekee?
Meneja wa bia ya Ndovu, Pamela Kikuli alisema “Ndovu ina kiungo cha kipekee ambacho wanywaji wachache wa Ndovu wanakifahamu. Ni kimea angavu, Crystal Malt ambavu ambacho hakipatikani ndani ya bia nyingine hapa nchini.

Kiungo hiki, crystal malt kimeandikwa kwenye nembo ya chupa ya Ndovu lakini watu wengi hawajaweza kutambua hilo. Kwa hiyo kwa kumsiadia mpenzi wa bia hii kufahamu kiungo hicho, kampeni mpya ya Ndovu ambayo tumeizindua hii leo inakusudia kumuwezesha mnywaji wa ndovu kutambua kiungo hiki kwa kutumia lenzi.


Gaudence Mkolwe, mpika bia mkuu wa kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) alisema “Crystal malt ni kiungo ambacho kiko ndani ya Ndovu na ndicho kinachoipa bia hii rangi yake ya dhahabu iliyokela na ladha laini ya kipekee. Hapa TBL tunajivunia sana kutengeza bia ya kiTanzania yenye ubora na tukiongelea ubora ni sawa na ubora wa kimataifa”


Natalia Celani, Meneja masoko wa Ndovu amesema “ Kampeni hii itatangazwa kwenye magazeti, mabango na kwenye baa mbalimbali hapa nchini. Pia kuna tangazo la redio linaloelezea jinsi kimea hiki kinavyoifanya bia ya ndovu kuwa ya kipekee, hivyo fuatilia kampeni hii na kama una lenzi tazama kwa umakini kwenye chupa ya Ndovu ili uone kiungo kinachoipa ladha ya kipekee bia hii”.

No comments:

Post a Comment