Sunday, November 6, 2011

HASSAN SHARRIF NDIYE KINARA WA VODACOM TANGA CYCLE CHALLENGE 2011!

 Mshindi wa kwanza wa Kilomita 140 wa mbio za baiskeli za “Vodacom Tanga cycle Challenge “ Hassan Sharif akimaliza mbio hizo kwa kwa kutumia masaa 4.13.07 .ambapo mbio hizo zilianzia katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga hadi Hale na kurudi katika uwanja huo hapo jana.
Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga Seleboss Mustafa akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi laki moja na nusu Mshindi wa kwanza wa mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilomita 140,Hassan Sharif (kulia) mara baada ya kuibuka kidedea katika mbio hizo kwa kutumia muda wa masaa 4:13.07 wapili toka kushoto Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude na msimamizi wa mawakala kanda ya Kaskazini Michael Kasun.
Mwaandaaji wa Mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge Sophy Wakati akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu kushoto kabla ya mbio hizo kuanza,wa pili kutoka kushoto Buruhani Yakub ambae ni Mwandishi wa Habari wa Mwananchi Communication na Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.
Washiriki mbio za Vodacom Tanga Cycle Challenge kwa upande wa walemavu wakimaliza mbio hizo hapo jana mjini Tanga.
Baadhi ya washiriki wa mbio za baiskel za Vodacom Tanga Cycle Challenge wa kilometa 140 wakichuana vikali hapo jana mjini Tanga ambapo Hassan Sharif aliibuka mshindi kwa kutumia masaa 4:13.07 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi laki moja na nusu.
Naibu Meya wa Mkoa wa Tanga ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na uchumi, Seleboss Mustafa, (kushoto) akimkabidhi shilingi 75,000 mshindi wa tatu wa mbio za Vodacom Tanga cycle Challenge kwa upande wa Kilomita 140 Revocatus Sebastian, aliyetumia Masaa 4: 15.52 mashindano hayo yaliyoanzia katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga hadi Hale na kurudi katika uwanja huo ,wanaoshuhudia wapili kutoka kushoto ni Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude, Michael Kasun ambae ni msimamizi wa mawakala wa Vodacom kanda ya Kaskazini.


Kwa Hisani ya Vodacom Tanzania
HASSAN Shariff ametwaa ubingwa wa mashindano ya Mbio za baiskeli ya (Vodacom Tanga Cycle Challenge 2011)baada ya kumaliza mwendo wa umbali wa kilomita 140 akiwa mbele ya washiriki wengine.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya Wakati Sports Promoter na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania yalishirikisha makundi matatu ambayo ni ya baiskeli zilizotengenezwa maalumu kwa michuano ambapo washiriki walipita Wilaya za Muheza na Korogwe na kurejea Tanga mjini umbali wa kilomita 140.


Sharrif alitwaa ubingwa huo akiwa katika kundi la baiskeli maalumu za mbio hizo ambapo alimaliza michuano hiyo akiwa amekimbia kwa saa 4.13.07 na kufuatiwa na Juma Kashinde aliyetumia muda wa saa 4.14.52 wakati mshindi wa tatu alikuwa Revecatus Sebastian aliyemaliza akiwa amekimbia kwa saa 4.15.30.


Nafasi ya nne ilikwenda kwa Hamis Milikioni aliyekimbia kwa saa 4.28.08, Mathew Alberto alimaliza akiwa amekimbia kwa saa 4.35.06 huku Athumani Muya akikimbia kwa saa 4.38.07.


Kundi la baiskeli za kawaida lilianzia Tanga mjini kupitia Tanganyika Wilaya ya Muheza umbali wa kilomita 80 ambapo Kadushi Nkandi aliongoza kwa kutumia muda wa saa 1.56.00,Issa Kashinde alishika nafasi ya pili kwa kumaliza akiwa ametumia muda wa saa 1.57.12 huku Mohamed Bundala alitumia saa 2.15.13.


Baiskeli za miguu mitatu zilikuwa za kulizunguka jiji la Tanga ambapo aliyeongoza ni Jackson Kinyusa aliyekimbia kwa dakika 30.20 akifuatiwa na Mohamed Balozi dakika 32.16 huku Medrin Sabuni akishika
ushindi wa tatu kwa kukimbia kwa dakika 45.02.


Mgeni rasmi ,Mohamed Mustapher ambaye pia ni diwani wa Kata ya Nguvumali na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Tanga,aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuukumbuka mchezo wa baiskeli
na kuwaomba kuboresha zaidi mwakani kwani Tanga ni mkoa wenye vipaji vingi.


Mgeni huyo ambaye alimwakilisha Meya wa Jiji la Tanga alimkabidhi Shariff kiasi cha sh 150,000, Kashinde sh 100,000,Revocatus sh 75,000 wakati washindi wa kwanza katika makundi ya baiskeli za miguu mitatu
na za kawaida walizawadiwa sh 100.000,wa pili sh 75,000 wa tatu sh 50,000 huku washiriki wengine wakipewa kifuta jasho cha sh. 10,000 kwa kila mmoja.


Afisa Udhamini wa Vodacom,Ibrahim Kaunde alisema huu ni mwaka wa pili kwa Kampuni yake kudhamini mashindano ya baiskeli kwa Mkoa wa Tanga na Mwanza lengo likiwa ni kuimarisha mchezo huo katika maeneo hayo kwa kuwa unaonekana kupendwa zaidi.


“Kimsingi Vodacom imejikita kudhamini michuano ya baiskeli Tanga na Mwanza kutokana na ari na mwamko uliopo kama ambavyo tunavyodhamini riadha mkoani Kilimanjaro”alisema Kaunde.

No comments:

Post a Comment