Sunday, November 6, 2011

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI BARAZA LA IDD NA SWALA YA EID KITAIFA MSIKITI WA AL FAROUK DAR!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya Baraza la Eid El-Haj, baada ya swala ya Idd iliyofanyikaKitaifa kwenye Msikiti wa Al farouq Kinondoni jijiji Dar es Salaam leo Novemba 6.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal Wa pili (kulia) Rais Mstaafu wa Comoro, Mohammad Abdallah Sambi (kulia) Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Muhidin Mkoyogole na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, wakijumuika na waumini wa dini ya kiislam katika swala ya Eid El Haj, iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd katika Msikiti wa Al Farouk, uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akimpokea Rais Mstaafu wa Comoro, Mohammad Abdallah Sambi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akipokelewa na mmoja wa waumini wa dini ya Kiislam, Asha Baraka, wakati alipowasili alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya Kiislam kuomba dua baada ya swala ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa aL Farouk Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliohudhulia swala ya Idd El Haj, baada ya kumalizika kwa swala hiyon iliyofanyika katika msikiti wa Al Farouk uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Novemba 6. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.

Na Theeastafrica Bloger
Waumini wa dini ya Kiislamu nchini leo wameungana na waislam wengine kote duniani kusherehekea sikukuu ya Idd El Haji baada ya baadhi yao kusafiri hadi mji Mtukufu wa Mecca kwenda kutekeleza ibada ya Hija.



Kitaifa swala ya Eid El Haji ilisaliwa katika Msikiti wa AL FAROUQ uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo Makamu wa Rais DK MOHAMED GHARIB BILAL alikuwa mgeni Rasmi. Akizungumza mara baada ya swala hiyo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ALHAD MUSSA SALUM ameupongeza uamuzi wa serikali wa kukataa kuhalalisha ndoa za mashoga na za jinsia moja.


Mara baada ya kumalizika Swala Eid lilifuata Baraza la Eid El Haji, Akizungumza kwenye baraza hilo Makamu wa Rais DK MOHAMED BILAL ametoa wito kwa wanaokwenda Hija kukumbuka kwamba hiyo ni ibada maalum hivyo wasiichanganye na masuala ya kisiasa.


Kwa upande wake Kaimu Mufti wa Tanzania Sheikh MUHIDIN MKOYOGORE amewaomba viongozi nchini kuongoza kwa kusikiliza matakwa ya wananchi ambapo amesema haki na uadilifu vikikosekana katika jamii husababisha vurugu na uvunjifu wa amani.

No comments:

Post a Comment