Sunday, November 6, 2011

MAMA ZAKHIA BILAL AZINDUA KUNDI NA ALBAM YA KWAANZA YA T-MOTO!

Waimbaji wa bendi ya Mapacha Wa3 kutoka (kushoto) Kalala Junior, Jose Mara na Khalid Chokoraa, wakishambulia jukwaa wakati walipokuwa wakisindikiza uzinduzi wa Kundi la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku Nov 4.

Mkurugenzi wa Kundi la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ‘Real Madrid’, Amin Salmin, akizungumza jukwaani wakati wa uzinduzi wa kundi hilo, uliofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akivuta utepe kuzindua rasmi kundi jipya la Taarab la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ‘Real Madrid’ wakati wa uzinduzi wa kundi hilo na albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akipokea zawadi ya Cd za kundi la T-Moto, kutoka kwa Mkurugenzi wa kundi hilo, Amin Salmin, baada ya Mama Zakhia kuzindua rasmi kundi hilo jana usiku kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
Mama Zakhia Bilal, Mama Tundu Pinda, Mama Kawawa, wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kundi la T-Moto baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mgeni Rasmi Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akizungumza jukwaani baada ya kuzindua rasmi kundi na albam ya kwanza ya kundi jipya la Tanzania Modern Taarab (T-Moto) uzinduzi uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam juzi Usiku Nove 4. 
Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Bi Mwanahawa Ally, akiimba jukwaani kibao chake cha Aliyeniumba Hajanikosea, wakati wa uzinduzi wa Kundi na albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam juzi usiku Nov 4.
Msanii wa kundi la Tanzania Modern Taarab, Mrisho Rajab, akiimba jukwaani kibao chake cha Mchimba Kaburi Zamu yake Imefika, wakati wa uzinduzi wa Kundi na albam ya kwanza ya kundi hilo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam juzi usiku Nov 4. Picha zote na www.sufianimafoto.blogspot.com

No comments:

Post a Comment