Wednesday, November 16, 2011

MKAZI WA KOTA ZA NHC MBURAHATI ALALAMIKIA KITENDO CHA JIRANI YAKE KUMDHULUMU NYUMBA!

Mkazi wa kota za Mburahati National Housing Bi LEAH RAMADHANI TUMBO amelalamikia kitendo cha madalali wa mahakama kuvunja, kuiba na kutoa vyombo vyake kwenye nyumba yake namba 508 aliyerithishwa na marehemu mume wake.

Akizungumza kwa masikitiko wakati vitu vyake vikiwa nje ya nyumba yake anayodai kuimiliki kihalali BI LEAH amesema jirani yake ambaye alipewa idhini ya kuinunua nyumba hiyo anadai mahakamani kwamba nyumba hiyo ni ya kwake ingawa hana hati miliki.


Mwenyekiti wa Mtaa huo amezungumza na kituo hiki kwa njia ya simu na kukiri kuletewa barua ya kutekelezwa kwa agizo hilo lakini hakutoa idhini ya kuvunja kwa kuwa suala hilo tayari lilikuwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment