Wednesday, November 16, 2011

MGOMO WA DALADALA KIGOGO WAINGIA SIKU YA PILI!

Umoja wa Madereva na Makondakta wanaotoa huduma ya usafiri barabara ya Kigogo jijini Dar es Salaam umesema licha ya serikali kuonesha nia ya kukarabati eneo korofi la Landa Bar hawatasitisha mgomo wao hadi eneo hilo litakapotengenezwa.

Akizungumza na kituo hiki Mwenyekiti wa umoja huo Bw AZIZI DAUDI amesema baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam SAID MECKY SADICK kutembelea eneo la tukio, mitambo ya ujenzi imefikishwa na kuegeshwa bila utekelezaji kuanza.


Mgomo huo wa Madereva na Makondakta wanaotoa huduma ya usafiri barabara ya Kigogo umeingia siku ya pili baada ili kuishinikiza serikali kulikarabati eneo korofi ambalo limekuwa likiharibu magari yao.

No comments:

Post a Comment