Thursday, November 3, 2011

MEMBE ATOA MSIMAMO WA SERIKALI 'HATURUHUSU MASHOGA HATA KAMA WAHISANI WATAKATAA KUTOA MISAADA KWA TANZANIA'!

Serikali imesema iko tayari kukosa misaada kutoka kwa nchi wahisani ambazo zimetishia kusitisha misaada yake kwa Tanzania ikiwa haitakubali kuhalalisha kufanyika kwa ndoa za jinsia moja maarufu kama za mashoga.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa BENARD MEMBE amesema kwa Tanzania kukubali ndoa za mashoga ni sawa na kuvunja sheria ya nchi ya mwaka 1971 kifungu cha 9 kifungu kidogo moja kifungu cha 9 kifungu kidogo tatu.

Kuhusiana na vita inayoendelea kati ya majeshi ya Kenya na kikundi cha Kigaidi cha Al Shabab Waziri MEMBE anasema watakutana mjini Nairobi Novemba 20 mwaka huu ili kuzungumzia SUALA HILO.
Baadhi ya mashoga wakiwa nje ya Viwanja vya TGNP hivi karibuni kuhudhuria tamasha la kumi la Jinsia liliandaliwa na mtandao huo.

No comments:

Post a Comment