Monday, November 7, 2011

WAZIRI MAHADHI AWAOMBA WATANZANIA KUSHIRIKIANA KATIKA KUENDELEZA UCHUMI!

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi(kulia ) akiwa na Mchungaji, Dk. Bill Hybels ( kushoto ) wakimsikiliza Mratibu wa mkutano wa mafunzo ya Kuinua Uchumi, Ustawi wa Jamii na Uongozi Bora, mchungaji, Peter Mitimingi uliofanyika leo kwenye hoteli ya Blue Pearl – Ubungo Plaza jijini Dares Slaam.

Naibu Waziri huyo alifungua mkutno huo kwa niaba ya Makamu wa Rais,Gharib Bilal, ambapo alisisitiza kuwa suala la kuendeleza nchi linategemea juhudi za pamoja kutoka kwa watu mbalimbali na mashirika na kuongeza kuwa serikali itayafanyia kazi mapendekezo yatakayotokana na mkutano huo.

Wakati huohuo Dk. Hybels alisema ili kuweza kuondoa umasikini ni lazima kila mwananchi apate kibali halisi cha kumiliki ardhi ikiwemo kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuwapatia elimu . Picha na Magreth Kinabo – Maelezo.

No comments:

Post a Comment