Monday, September 19, 2011

WAKAZI WA MAGEUZI MANISPAA YA SHINYANGA WALALAMIKIA IDARA YA ARDHI!

Baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mageuzi kata ya Majengo Mapya Manispaa ya Shinyanga wamelalamikia kitengo cha Idara ya Ardhi cha Manispaa hiyo kwa kuwanyang’anya viwanja vyao walivyokuwa wakivitumia kwa muda mrefu kama mashamba na kuwapa wageni .

Wakizungumza na kituo hiki kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema idara ya ardhi inawapa viwanja watu wenye fedha na kuwanyanyasa wananchi ambao ndiyo walipaswa kupewa kipaumbele katika upimaji na ugawaji huo wa viwanja


Kwa upande wake Afisa Ardhi wa Manispaa ya Shinyanga ELIUS AUGUSTINO amekiri kuwepo kwa malalamiko hayo katika kata mbalimbali na kuwataka wananchi wavute subira wakati Serikali ikilifanyia kazi suala hilo.

No comments:

Post a Comment