Friday, September 2, 2011

VIJANA HAWAPENDI KUELIMISHWA KUHUSIANA NA ELIMU YA AFYA- PRINMAT!

Chama cha Wauguzi Wakunga Wasajiliwa walio katika huduma binafsi PRINMAT kimesema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni vijana nchini kutoona faida ya elimu ya afya ya uzazi inayofikiswa katika maeneo yao na waelimishaji rika.

Akizungumza wakati wa Mkutano wa wadau kwa lengo la kupeana mrejesho wa utekelezaji wa mradi wa vijana Katibu Mtendaji wa PRINMAT KEZIAH KAPESA amesema vijana wengi hususani wa maeneo ya vijijini wanachohitaji ni ajira na sio elimu ya afya.


Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Vijana kutoka NORVEST MATEE amesema kukamilika kwa mkutano huo kutawawezesha kuzifanyia kazi changamoto zitazojitokeza na kufanya maboresho zaidi ya mradi.

No comments:

Post a Comment