Monday, June 27, 2011

WALIOCHAKACHUA KURA ZA MAONI UDIWANI KUKIONA UCHAGUZI UJAO WA CCM: NAPE


NA BASHIR NKOROMO, LINDI


KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye amesema Chama kitawaadabisha bila huruma waliojihusiha na uchakachuaji wa kura za maoni ya wagombea wa udiwani katika uchaguzi mkuu uliopita.

Alisema viongozi hao lazima waadabishwe kwa kuchukuliwa hatua kwa sababu uchakachuaji huo, uliigharimu sana CCM kwa kuipatia matokeo mabaya katika baadhi ya kata na majimbo na hivyo kukipunguzia heshima yake pamoja na kwamba kilipata urais na viti vingi sana vya ubunge na udiwani kwa nchi nzima. Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Fisi katika Manispaa ya Lindi mjini, Nape alisema pamoja na wachakachuaji wasaliti wa Chama nyakati za uchaguzi nao hawatasalimika.


"Tunafahamu kuwa tunao viongozi na wanachama wetu wengi waandilifu na wasiothubutu kukisaliti chama hata siku moja, hawa tutawaenzi, lakini wenye tabia za usaliti na wachahachuaji wa kura za maoni kwa faida ya matumbo yao hawa lazima tutashughulika anao wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa Chama", alisema Nape.


Alisema, hatua za kuwashughulikia ni miongoni mwa maazimio yaliyopitishwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Taifa (NEC), kilichofanyika mjini Dodoma, Aprili mwaka huu, ambapo pia yalifanyika mabadiliko makubwa katika uongozi juu kwa lengo la kukirejesha Chama katika mustakabali kilioasisiwa nao. Nape alisema, kimsingi Chama kinachukua hatua hizo, kwa sababu kinatambua kuwa bila usaliti wa viongozi wachache kisingeweza kupoteza baahi ya majibo na kata katika uchaguzi mkuu uliopita ikilinganishwa na wingi wa wanachama kilio nao nchi nzima.


Alitoa mdano wa jimbo la Lindi mjini abalo limechukuliwa na upinzani, kwamba katika jimbo hilo kuna wanachama wengi wa CCM ikilinganishwa na vyama vingine vyote vya siasa, lakini kwa kuwa wapo waliokisliti Chama ndiyo sababu CCM ikashindwa katika jimbo hilo.


"Baada ya matokeo ya uchaguzi, wakati huo nikiwa mkuu wa wilaya nilipita hapa Lindi mjini nikaona watoto wakishangilia kushindwa CCM. Nikauliza mbona wanaoshangilia ni watoto wakubwa waliopiga kura wako wapi? nikajibiwa na wenyeji kwamba, waliopiga kura za kuiwezesha CUF kushinda ni wanachama wa CCM hivyo hawawezi kutoka barabarani kushangilia kushindwa chama chao",alisema Nape.


"Kwa hiyo inaonekana hapa na mahali pengi tuliposhindwa, kulikuwa na wanachama wenye tabia ya mipini ya shoka ambapo bila mipini hiyo ambayo ni miti shoka lisingekuwa na uwezo wa kukata miti mingine. Sasa tunasema tabia hii ikome..", alisema Nape.


Alisema, wapo ambao hukichukia Chama kutokana na kero mbalimbali, lakini wengi ni sababu ya kuendekeza njaa za matumbo yao, na kufafanua kwamba ikiwa yupo mwenye kero sasa milango ipo wazi kuzitoa kwenye ngazi zinazohusika kwa kuwa sasa chama kimefungua masikio kwa ajili ya kupokea kero na kuzishughulikia kuliko awali.Kuhusu wasaliti, Nape aliwataka kuchagua moja, kati ya kuachana na tabia hiyo kabla ya kushughulikiwa au kuhamia katika vyama wanavyotaka badala ya kujaza wingi wa idadi ya wanachama wakati ni mamluki.


Akizungumia kero ya uhaba wa maji Lindi mjini,Nape alisema, Serikali ya CCM inaitambua kero hiyo, na imefanya juhudi kujaribu kuitatua mojawapo ikiwa ni mradi wa maji bwawa la Kidunda ambao kukamilika kwake kutamaliza kabisa tatizo la maji katika eneo hilo. Nape alisema hata hivyo, ili maji yaweze kufika Lindi maji kutoka kisima hicho yanatakiwa kusukumwa na pampu ya mashine za umeme ambao utakwenda kisimani na kwamba licha ya nguzo kuwepo tayari lakini umepekwaji umeme eneo hilo umekumbwa na changamoto baada ya kushindikana kupitisha nguzo hizo katika mashamba ya wananchi ambao wanahitaji fidia.


Nape aliwaagiza viongozi na watendaji wa serikali wa mkoa wa Lindi, kwenda kuwashawishi wananchi wakubali kupitisha nguzo kwa kuandikiana mkataba wa malipo na serikali pindi fedha zitakapopatikana. Alisema, ni lazima viongozi wa CCM waende kwa wananchi hao wawelimishe umuhimu wa kupitishwa nguzo hizo ili maji yafike Lindi mjini, kwa kuwa hatua ya kutaka mpaka wapate fidia japoinawezekana lakini itachukua muda mrefu wakati wananchi wanaendelea kuteseka kwa ukosefu wa maji.


Jana, Nape ambaye anafuatana na Mjumbe mwenzake wa NEC, anayeshughulikia Idara ya oganaizesheni, Asha Abdalla Juma na Katibu Mkuu Msaidizi wa Idara ya Itikadi na Uenezi Taifa, sixtus Mapunda alimaliza ziara ya siku mbili mkoani humo, na alitarajiwa kuendelea na ziara ya nyingine ya siku mbili mkoani Mtwara kwa siki mbili.

No comments:

Post a Comment