Saturday, September 10, 2011

BREEEEEAKING NEWS! MELI YA MV SPICE ISLANDER YAZAMA ENEO LA NUNGWI IKIWA NA ABIRIA 500!

Meli ya MV Spice Islander imezama baada ya kuondoka katika banadari ya Zanzibar. Iliondoka Zanzibar kwenda Pemba saa 4.20 Usiku na kuzama katika eneo la Nungwi nje kidogo ya bandari ya Zanzibar.

Akizungumza na Theeastafrica Afisa Uhusinao wa SUMATRA DAVID MZIRAY amesema Meli hiyo iliyoanzia safari yake kwenye bandari ya Dar es Salaam ilitia nanga salama kwenye bandari ya Malindi Zanzibar kabla ya kuondoka kuelekea Pemba.

Akifafanua MZIRAY alisema ikiwa eneo la Nungwi meli hiyo ilipigwa na dhoruba katika mkondo wa bahari wa eneo hilo ambao ni mkali na wenye uwezo wa kuangusha hata meli kubwa. Katika juhudi za uokoaji majeruhi na miili ya watu waliopoteza maisha katika meli hiyo meli ya MV Jitihada imeelekea eneo la tukio ikiwa na Kikosi cha KMKM wakiwa na chombo chao kwa ajili ya kwenda kutoa msaada kwenye eneo la tukio.


Taarifa zaidi zinasema Meli hiyo iliyoanzia safari yake kwenye Bandari ya Dar es Salaam ilikuwa na abiria 500 na wafanyakazi 12. Meli hiyo iliyozama imesajiliwa na Mamlaka ya Meli Zanzibar na kwamba taarifa za tukio hilo zilikifikia kituo cha ufuatiliaji na ukoaji MRCC saa 9.10m usiku ambapo taarifa hizo pia zilifikishwa pia kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Kikosi cha Polisi Wanamaji Zanzibar.

Akizungumza na blog hii ya jamii Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP SAID MWEMA amesema tayari vikosi vya uokoaji vimeenda kwenye eneo hilo kwa msaada wa helkopta ili kupata miili ya majeruhi na maiti zilizookolewa.

Baadhi ya mashuhuda wamesema majeruhi wamepelekwa kwenye Hospitali ya Maisara mjini Zanzibar ambao wanapatiwa matibabu na kwamba ndugu na jamaa wapo katika eneo hilo kwa ajili ya kutambua maiti ya ndugu zao. Kwa kuwa ajali hiyo imetokea eneo la Nungwi imeelezwa kwamba wati wote hawatapekwa Pemba na badala yake wataletwa katika eneo hilo kutokana na ukaribu kwa ajili ya kuwapatia wahanga huduma.

Mmoja wa ndugu anasema kwa upande wa wakazi wa Pemba na Zanzibar tukio hilo limeleta msiba mkubwa kutokana na idadi ya watu wengi waliokuwemo kwenye Meli hiyo wanaodaiwa kufikia zaidi ya 1000.

3 comments:

  1. Mungu awalaze mahali pema peponi marehemu wote na awape heri na baraka majeruh waliolazwa
    INNALILLAH WAINNAILLAH RAJIUN..Mungu awalaze mahali pema peponi marehemu wote na awape heri na baraka majeruh waliolazwa
    INNALILLAH WAINNAILLAH RAJIUN..

    ReplyDelete
  2. Serikali ikilifumbia macho suala hili basi roho za watu zinaweza kubadilika mara moja kwani pamoja na mipango na muandiko wa m. mungu lakini kuna uzembe wa wafanyakazi wa shirika la Bandari hasa ukizingatia kabla ya meli kuondoka ilionekana ikiwa katika hali mbaya sana imelala upande mmoja hali iliyohatarisha masiha ya watu na baadhi yao walisikia wakipiga kelele wekeni ngazi tuteremke mtatuuwa jami kwa hili bila ya huruma na kuungalia huyu ni nani na huyu ni wanani serikali itoe adhabu kali kwa wahusika wa uzembe uliosababisha kupotea maisha ya watu

    ReplyDelete
  3. Serikali ikilifumbia macho suala hili basi roho za watu zinaweza kubadilika mara moja kwani pamoja na mipango na muandiko wa m. mungu lakini kuna uzembe wa wafanyakazi wa shirika la Bandari hasa ukizingatia kabla ya meli kuondoka ilionekana ikiwa katika hali mbaya sana imelala upande mmoja hali iliyohatarisha masiha ya watu na baadhi yao walisikia wakipiga kelele wekeni ngazi tuteremke mtatuuwa jamani, kwa hili bila ya huruma na kuungalia huyu ni nani na huyu ni wanani serikali itoe adhabu kali kwa wahusika wa uzembe uliosababisha kupotea maisha ya watu

    ReplyDelete