Saturday, September 10, 2011

HAYA NDIYO YALIYOJIRI KUHUSIANA NA TUKIO ZIMA LA AJALI YA MV SPICE ISLANDER!

                                                     TUKIO LILIANZA KAMA HIVI
Meli iliyozama inaitwa MV Spice Islander. Iliondoka Zanzibar kwenda Pemba saa 4.20 Usiku na kuzama katika eneo la Nungwi nje kidogo ya bandari ya Zanzibar. Meli ya MV Jitihada imeelekea eneo la tukio, Kikosi cha KMKM kikiwa na chombo chao nacho kinaelekea eneo la tukio.


Meli hiyo iliyoanzia safari yake kwenye Bandari ya Dar es Salaam ilikuwa na abiria 500 na wafanyakazi 12. Meli hiyo iliyozama imesajiliwa na Mamlaka ya Meli Zanzibar na kwamba taarifa za tukio hilo zilikifikia kituo cha ufuatiliaji na ukoaji MRCC saa 9.10m usiku ambapo taarifa hizo pia zilifikishwa pia kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Kikosi cha Polisi Wanamaji Zanzibar.

     SAFARI YA WAKAZI JIJINI DSM HADI UNGUJA KUFUATILIA HALI YA JAMAA ZAO!
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wamendelea kusafiri kuelekea mjini Unguja kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao waliojeruhiwa au kufa kutokana na ajali ya meli ya Spice Islander iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Meli hiyo iliyotoa nanga kwenye bandari ya Zanzibar majira ya saa 4.20 usiku ikielekea Pemba ilizama katika eneo la mkondo wa Nungwi nje kidogo ya bandari ya Zanzibar.

Mwandishi Wetu SALEHE MASOUD ambaye yupo kwenye boti akielekea Zanzibar kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo amezungumza na baadhi yak abiria ili kupata maoni yao kuhusiana na ajali za mara kwa mara kwa vyombo vya usafiri vinavyoelekea Zanzibar.

                    ZOEZI LA UOKOAJI LAENDELEA KWA NJIA YA HELKOPTA
Wakati zoezi la uokoaji wa majeruhi na maiti kutokana na ajali ya Meli ya MV Spice Islander likiendelea Jeshi la Polisi nchini limesema litatoa taarifa rasmi kuhusiana na tukio zima la kuzama kwa meli hiyo iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 500.
Akizungumza na kituo hiki Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP SAID MWEMA amesema tayari meli na helikopta zilizofika kwenye eneo la tukio zimeshaanza kazi na takribani watu 260 wameokolewa.


Meli hiyo iliyozama katika eneo la mkondo wa Nungwi Unguja majira yak saa tisa usiku baada ya kukumbwa na dhoruba iliondoka kwenye bandari ya Zanzibar saa 4.20 usiku tayari kuelekea Pemba.


ABIRIA WALIOKUWA WAKITOKEA JIJINI DSM WAZUILIWA KUPISHA MAJERUHI NA MAITI KUSHUSHWA KUTOKA NUNGWI!
Baadhi ya abiria waliokuwa wakitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea mjini Unguja kufuatilia hali ya ndugu na jamaa zao waliokuwa kwenye Meli ya MV Spice Islander iliyozama kwenye eneo la Mkondo wa Nungwi wamezuiliwa kushuka kupisha kazi ya kushusha majeruhi kutoka kwenye meli mbili zilizoenda eneo la tukio kuokoa abiria.


Mwandishi wa kituo hiki SALEHE MASOUD ambaye ni mmoja wa abiria kwenye boti hiyo anaelezea hali halisi ilivyo katika eneo la bandari ya Malindi Zanzibar.

VIKOSI VYA KMKM VYAFANIKIWA KUOKOA WATU 267 NA MAITI WANANE
Vikosi vya uokoaji vya KMKM, JKU na kituo cha Ufuatiliaji na Ukoaji MRCC kinachoongoza zoezi la uokoaji majeruhi na miili ya watu waliokufa kwa ajali ya meli ya Meli ya MV Spice Islander iliyozama kwenye eneo la Mkondo wa Nungwi vimefanikiwa kupata majeruhi 268 na maiti nane.
Akizungumza na kituo hiki kutoka viwanja vya Maisara mjini Unguja Mwandishi wa Kituo hiki SALEHE MASOUD amesema vikosi hivyo vinavyoongozwa na helkopta mbili vinaendelea na zoezi hilo na kwamba kinachosubiriwa ni boti moja ya uokoaji iliyoenda kufuata majeruhi wengine kutoka eneo la tukio.


Eneo hilo ulipo sasa hivi kuna kiongozi yeyote unayeweza kutupatia ili tuzungumze naye kupata taarifa zaidi la tukio hilo? Asante kwa taarifa hizo na tutakupigia tena baadae hasa kama utabahatika kuzungumza na majeruhi yeyote kupata taarifa zaidi.
                                    Baadhi ya mabaharia wakiokoa baadhi ya mizigo wa MV Spice.

No comments:

Post a Comment