Friday, August 26, 2011

MEYA SLAA KULA EID EL IFTAR NA WATOTO YATIMA!


Na Hadija Chumu, Maelezo
Taasisi mbalimbali zimeombwa kutoa ufadhili wa vifaa au fedha kwa ajili kufanikisha tafrija ya chakula cha pamoja kwa watoto wa mitaani na yatima ambayo itafanyika tarehe 31 Agosti 2011 katika Kituo cha Kulelea Yatima cha Tushikamane kilichopo Tabata Bima

Hayo yamesemwa na Katibu wa Kamati ya maandalizi ya Mfuko wa Watoto wa Mitaani wa Ali Hassan Mwinyi Omari Njani alipozungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam jana(leo) ambapo mgeni rasmi atakuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mheshimiwa Jerry Silaa


Bwana Njani alisema wameandaa tafrija ya kusheherekea sikukuu hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa kuwahudumia Watoto walio katika Mazingira Hatarishi na Yatima wa Tushikamane ili kushiriki na kuonyesha upendo na watoto wa Mtaani na Yatima

Alisema mpaka sasa jumla ya shilingi 6,890,000 kinahitajika kwa ajili ya maandalizi ya tafrija ya kusheherekea Sikukuu hiyo kwa mwaka huu. Aliwataja wageni wengine ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Leonidas Gama,Mbunge wa jimbo la Segerea Dk. Milton Mahanga ,Vijana na watoto kutoka katika kituo cha Alli Hassan Mwinyi


Wengine ni wasichana wanaoishi katika mazingira magumu kutoka kituo cha KIWOHEDE,Vijana kutoka Chama cha Songa Mbele (SOMBEPA), vyombo vya Habari na taasisi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment