Monday, July 11, 2011

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WATENDAJI WA UHAMIAJI WANAOGHUSHI UTOAJI PASSPORT!

Serikali imesema imekuwa ikiwachukulia hatua kali watendaji wa idara ya uhamiaji ambao wanahusika na utoaji wa pasipoti kwa Raia ambao sio wa wa Tanzania.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu wa Waziri Mambo ya ndani KHAMIS KAGASHEKI wakati alipokuwa akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa viti maalum kupitia CCM ESTER BULAYA.


Akijibu swali hilo Naibu waziri huyo amekiri kuwepo kwa watendaji ambao ni wabadhirifu katika idara hiyo na kuongeza kwamba serikali imekuwa ikichukua hatua za haraka kwa watumishi ambao wamethibitika kujihusisha na utoaji wa Pasipoti kinyeme na sheria za nchi.

No comments:

Post a Comment