Monday, July 11, 2011

ONGEZEKO LA WATU DUNIANI LACHANGIA MABADILIKO YA TABIA NCHI!

Wakati leo Tanzania ikiungana na nchi nyingine ulimwenguni kuadhimisha siku ya Idadi ya Watu Duniani, imebainishwa kuwa ongezeko hilo limekuwa moja ya sababu zinazochangia kasi ya uharibifu wa mazingira nchini kutokana na jamii nyingi kutegemea mazingira kama njia ya kukuza na kuendeleza uchumi wa Taifa.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kutathimini Rasilimali za Taifa (IRA), Profesa AMOS MAJULE, amesema ipo haja ya kupunguza kasi ya vitu vinavyochangia uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na jamii kuendelea kuelimishwa zaidi juu ya utunzaji wa mazingira.


Aidha maadhimisho hayo ambayo kitaifa yamefanyika Mkoani Tanga yameambatana na kauli mbiu “Fursa na Changamoto za ongezeko la Idadi ya Watu katika uchumi”.

No comments:

Post a Comment