Monday, July 11, 2011

TABOA YAENDELEA NA MSIMAMO WA KUGOMEA MATUMIZI YA KIFAA CHA U-TRACK!

Chama cha wamiliki wa mabasi yaendayo Mikoani TABOA kimepanga kutoendelea na utoaji wa huduma ya usafiri kwa wananchi iwapo serikali itaendelea na mpango wake wa kushinikiza ufungwaji wa kifaa cha kufuatilia mwenendo wa safari unaotambulika kama U-TRACK

Katibu Mkuu wa TABOA Enea Mrutu amesema serikali inapaswa kuweka utaratibu wa kutumia kifaa cha kufuatilia mwenendo wa safari wa CAR TRACKSYSTEM hadi pale itakapothibitika kwamba wamiliki wamekuwa na uelewa wa kutosha kuhusu Mfumo mpya wa U-TRACK kuliko kuweka shinikizo la ufungwaji wa kifaa hiko


Kwa upande wa Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Kamanda MOHAMED MPINGA amesema swala la mgomo unaopangwa kufanywa na wamiliki hao sio suluhisho jambo la msingi kwa wamiliki hao ni kusubiri maamuzi ya kamati ya baraza la taifa usalama barabarani litakaloketi hii leo na kujadili namna ya kutanzua mzozo huo
Nae Mkurugenzi Mkuu wa mfumo wa U-TRACK, ZULL MOHAMED amesema kampuni yake iliingia mkataba halali na TABOA hivyo inasubiri maamuzi kutoka katika Tume ya kamati ndogo iliyoteuliwa ili kuangalia namna mchakato huo utakavyokuwa.

No comments:

Post a Comment