Sunday, July 10, 2011

MWANANYAMALA SOKONI WAULALAMIKIA MTAA WA KWA KOPA KUJENGA CHOO KWENYE ENEO LAO!

Uongozi wa Soko la Mwananyamala, Jijini Dar es salaam, umelalamikia hatua ya Serikali ya mtaa wa kwa Kopa kujenga choo katika eneo lao bila idhini ya uongozi huo.

Akizungumzia ujenzi huo Mwenyekiti wa Soko la Mwananyamala, HAMIS MARANDE, amesema pamoja na Uongozi kupeleka taarifa Wilayani ikiwa ni pamoja na kukaa na Uongozi wa mtaa wa kwa komba bado hakuna hatua zozote zilizochukuliwa katika kutatua tatizo hilo.


MARANDE, amesema kuwa haelewi dhumuni la ujenzi huo wakati Mtaa wa kwa komba una maeneo mengi ya wazi ambayo yanaweza kutumiwa katika ujenzi wa choo na kwanda hatua hiyo inaweza kusababisha mgogoro baina ya wakazi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment