Sunday, July 10, 2011

BAADHI YA WANANCHI WALALAMIKIA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA YA TAA!

Baadhi ya wananchi waishio vijijini wamelalamikia hatua ya serikali kupandisha gharama ya mafuta ya taa katika bajeti yake kufuatia kuwepo kwa uwezekano wa ongezeko hilo kuathiri watu wenye kipato cha chini.

Wamesema familia nyingi vijijini hazina umeme hali inayosababisha zitegemee zaidi mafuta hayo nyakati za usiku ikiwa ni pamoja na matumizi kwa watoto wao waliopo mashuleni hasa wale wanaokaribia kufanya mitihani yao ya taifa.


Wamesema ingawa nia ya serikali ilikua ni kuweka uwiyano baina ya mafuta ya taa na petroli kwa kudhibiti uchakachuwaji lakini wameishutumu kwa kutofanya utafiti wa athari za kupandisha bei ya mafuta hayo.

No comments:

Post a Comment