Tuesday, July 26, 2011

MH. ANNE KILANGO MALECELA ALIA NA SERIKALI KUWAPANGIA BEI WAKULIMA NCHINI!

                                                         Mama ANNE KILANGO MALECELA

Mbunge wa Same Mashariki Mama ANNE KILANGO MALECELA amehoji uhalali wa serikali kuwakataza wananchi kuuza mazao katika soko wanalolitaka, wakati ilishatangaza kwamba haitajihusisha na biashara ikiwemo kushindwa kuwasaidia katika kupata pembejeo na miundombinu bora.

Akifafanua Mheshimiwa ANNE KILANGO amesema, chakula ni cha wakulima na anapinga kitendo cha serikali kutaka kuwapangia bei ya mazao yao wakati hata ile iliyopo haikidhi gharama za uzalishaji.


Katika hatua nyingine KILANGO alikemea tabia ya baadhi ya Mawaziri kutoa ahadi zisizotekelezeka wanapowatembelea wananchi katika maeneo yao jambo linaloiondolea uaminifu serikali kwa jamii.

No comments:

Post a Comment