Tuesday, July 26, 2011

MBUNGE WA KOROGWE MJINI ADAI MAFAO YA WAKULIMA WA SHAMBA LA NGOMBEZI!

Mbunge wa Korogwe Mjini kupitia CCM, YUSUPH NASSIR amehoji lini serikali itawalipa haki zao waliokuwa wafanyakazi wa shamba la Mamlaka ya Mkonge Ngombezi na mengineyo ambao mpaka sasa wameachwa kwa unyonge bila majibu yoyote.

Akichangia Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Mheshimiwa NASSIR amesema wawekezaji wa Katani Limited ambao walimilikishwa Ngombezi na mamlaka ya mkonge walishindwa kuliendeleza shamba hilo na hatimaye kulirudisha serikalini bila kuwalipa wakulima mafao yao.


Kuhusiana na matrekta yaliyoletwa kwa ajili ya kusaidia mkakati wa serikali wa kilimo kwanza aliomba serikali itoe fedha kwa jimbo lake ili wakanunua matrekta yao kwa Dola Elfu Tisa (9,000/-) badala ya shilingi milioni 38 hadi 40 ya sasa.

No comments:

Post a Comment