Wednesday, July 13, 2011

MAENDELEO YA AFRIKA YATALETWA NA WAAFRIKA WENYEWE-DK BILAL!


Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. MOHAMMED GHARIB BILAL, amebainisha kuwa maendeleo ya bara la Afrika hayana budi kuletwa na waafrika wenyewe kupitia rasilimali mbalimbali zinazopatikana katika bara hilo.

Dkt. BILAL ameeleza hayo wakati wa Mkutano wa Baraza la Afrika linaloshughulika na elimu ya masafa (ACDE), unaoendelea Jijini Dar es salaam, kwa lengo la kubadilishana mawazo na uzoefu katika utoaji wa Elimu Huria ambao unatarajiwa kuhitimishwa julai,15 mwaka huu.


Amesema kuna haja ya Waafrika kujiwekea mikakati madhubuti katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana na kuondokana na utegemezi kutoka kwa mataifa wahisani.


Katika hatua nyingine Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. SHUKURU KAWAMBWA, amesema Serikali imeazimia kuimarisha udhibiti katika Elimu mtandao kupitia tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu hiyo nchini.


Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu huria Tanzania, Prof. TOLLY MBWETTE, amesema tatizo linalokikabili chuo hicho kwa sasa ni kukosa maombi ya kutosha ya udahili kwa wanafunzi walioko mikoani hususani wale wa masomo ya Sayansi.

No comments:

Post a Comment