Wednesday, July 13, 2011

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YADHAMINI MKUTANO WA JUKWAA LA WAHARIRI KWA ZAIDI YA MILIONI 168/-

 

Jukwaa la Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini TEF kwa kushirikiana na Kampuni ya Bia ya Serengeti SBL wameandaa mkutano wa Kitaaluma wa wahariri utakaofanyika Arusha kuanzia Julai 14 hadi Julai 17 mwaka huu.

Akizungumzia Mkutano huo, Katibu wa Jukwaa la Wahariri wa Vyombo vya habari nchini TEF, NEVILLE MEENA amewakumbusha wahariri wa vyombo vya habari nchini kuwa na msimamo mmoja wakati wanapotetea masilahi ya taifa na wananchi kwa ujumla na utofauti wao uwe katika kuwasilisha hoja.


Mkutano huo utakaowashirikisha wahariri 80 wakiwemo 65 kutoka Bara na 15 wa Tanzania Visiwani umedhaminiwa na SBL kwa zaidi ya shilingi milioni 168 na mada yake kuu itakuwa Undishi wa Habari unaozingatia Wajibu.
Wakati huohuo Timu ya Jukwaa la Wahariri Tanzania ‘TEF STARS ‘ Jumamosi ya Julai 16 mwaka huu itajitupa katika Uwanja wa TPC uliopo mjini Moshi kupimana nguvu na Timu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti ikiwa ni moja ya shamrashamra za uzinduzi wa kiwanda kipya cha kampuni hiyo kilichopo mjini humo.

Meneja wa Timu ya TEF STARS ambaye pia ni Mhariri wa Gazeti la Spoti Starehe MASOUD SANANI amesema ili kuonesha uwezo wa wahariri wa vyombo vya habari nchini watatumia mtindo wa TOTAL kulishambulia lango la SBL katika kipindi chote cha mchezo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL TEDDY MAPUNDA amesema kwa kuwa Serengeti itawalewesha wachezaji hao wa TEF STARS suala la ushindi kwao si tatizo.PICHA NA MO BLOGS.

No comments:

Post a Comment