Thursday, June 9, 2011

WANAFUNZI DUCE WAANDAMANA LEO HII HADI BODI YA MIKOPO KUDAI FEDHA ZA BAJETI YA MWAKA 2010/2011 ZILIZOKWAPULIWA!

                             Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo GEORGE NYATOGO
Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) wameandamana hadi Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) kuhoji kitendo cha bodi hiyo kutowaingizia fedha zao za mikopo ambapo zilitengwa na serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2010/2011.

Wakizungumza kwenye mkutano na baadhi ya viongozi wa Bodi hiyo wanafunzi hao wamepinga kitendo cha Bodi ya Mikopo kushindwa kuwaingia fedha zao za mkopo, wakati zilikwishatolewa na serikali katika mwaka wa fedha uliopita.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti wa Bodi hiyo ASANGE BANGU amesema tatizo kubwa lililochangia kuwepo kwa mvutano huo ni kitendo cha baadhi ya wanafunzi kuhama kutoka chuo kimoja hadi kingine wakati bodi hiyo ikiwa haijataarifiwa kubadilisha kiasi cha mkopo.

No comments:

Post a Comment