Thursday, June 9, 2011

TRAWU KUMFUATA PINDA BUNGENI KUDAI MKATABA MPYA WA HALI BORA!

                                    Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw BAKARI KISWALA
Chama Cha Wafanyakazi wa Reli nchini ( TRAWU), kinatarajia kuonana na Waziri Mkuu, MIZENGO PINDA kufuatia madai ya mkataba mpya wa hali bora pamoja na nyongeza ya kifuta jasho kutopatiwa ufumbuzi.

Akizungumza wakati wa kikao cha Wafanyakazi wa Shirika la Reli nchini (TRL), Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho, Bw BAKARI KISWALA, amesema wamelazimika kuonana na Waziri PINDA, kufuatia madai hayo kutofanyiwa kazi tangu Mkataba huo ulipoisha Machi 31, mwaka huu.
Katika hatua nyingine, chama hicho kimemtangaza Bwana CHRISTOPHER KAZIYO, kukaimu nafasi ya katibu Mkuu iliyoachwa na Marehemu SILVETER RWEGASIRA, aliyefariki dunia April 4 mwaka huu, mpaka uchaguzi mkuu wa chama hicho utakapofanyika mwishoni mwa Julai mwaka huu.

No comments:

Post a Comment