Wednesday, June 22, 2011

WAKAZI JIJINI WAOMBA BARABARA YA SAM NUJOMA MAJEMBE IPANULIWE!

Baadhi ya wakazi jijini Dar es Salaam wameiomba Manispaa ya Kinondoni kuipanua barabara ya Sam Nujoma kona ya Majembe ili kuepusha ajali za mara kwa mara zinazotokea katika eneo hilo.

Wakizungumza na kituo hiki wakazi hao wamesema kutokana na wembamba wa barabara hiyo unaochangiwa na mashimo pamoja na mmomonyoko wa udongo Manispaa ya Kinondoni haina budi kulipanua eneo hilo ili liweze kupitika kwa urahisi.
Uchunguzi uliofanywa na CLOUDS FM umegundua kuwa kila baada ya takribani siku tatu ajali za magari na bajaj zimekuwa zikitokea katika kona ya Majembe barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam hivyo kusababisha vifo pamoja na majeruhi kwa baadhi ya madereva.

No comments:

Post a Comment