Thursday, June 23, 2011

ZIARA YA NAPE NNAUYE KAMPUNI YA TSN NA TBC!

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akijibu maswali ya mtangazaji wa TBC Taifa, Joyce Kingalame alipotembelea studio za kituo hicho, Mikocheni mjini Dar es Salaam, jana. Kushoto pia ni mtangazaji wa kituo hicho, Shaaban Kisu.
KATIBU wa Halmashuri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kulia) akizungumza na wasanii wa kundi la Orijino Komedi, katika studio za kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC1), alipofanya ziara katika kituo hicho jana. Kutoka kushoto ni Mjuni Sylivery (Mpoki), Sekioni David (Seki) Lucas Mhuvile (Joti) na Emmanuel Mgaya (Masanja).
Kaim Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN), Mkumbwa Ally akiwatambulisha viongozi wa kampuni hiyo, kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,CCM nape Nnauye (kushoto) alipotemblea Ofisi za TSN mjini Dar es Salaam, leo. Wengine kutoka kushoto ni Mhariri Mkuu wa habarileo, Joseph Kulangwa na Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa TSN, Sukulu Magesa.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa ngazi za juu wa Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers(TSN), kwenye ukumbi wa Ofisi za kampuni hiyo, mjini Dar es Salaam, leo. Viongozi hao kutoka kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Mkumbwa Ally, Meneja Rasilimali watu na Utawala, Sukulu Magesa na Mhariri Mkuu wa Habari Leo, Joseph Kulangwa.

Nape akionyeshwa maandalizi katika hatua za mwisho kabla ya habari kwenda mtamboni ambako pia hupokewa kwa mtandao kabla ya kuchapwa, alipokuwa katika ofisi za TSN. (Picha na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment