Monday, June 13, 2011

WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA KUTOKA JAPAN WAMALIZA MUHULA WAO!

Wafanyakazi wa kujitolea kutoka Japani (Japanese Overseas Cooperation Volunteers) kupitia shirika la JICA ambao wamemaliza muda wao wa kufanya kazi nchini watatembelea Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, tarehe 16 Juni, 2011 kabla ya kuondoka nchini.
Wataalamu hao ni watano na walifanya kazi kwa muda wa miaka miwili katika sehemu mbalimbali kama ifuatavyo;


- Bi. Sayaka HOSOYAMADA: Elimu ya Sayansi na Hisabati: Shule ya Sekondari ya Ngudu, Mwanza
- Bi. Yumi KOYAMA: Elimu ya Mazingira: Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mtwara
- Bi. Noriko KOMATSU: Uuguzi: Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea, Lindi
- Bi. Norie SASAKI: Elimu ya Watoto Wadogo: Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Mbeya
- Bw. Hayato WATANABE: Ufundi Magari: Chuo cha Ufundi Songea (VETA), Ruvuma


Katika ofisi ya UTUMISHI, kila mfanyakazi atatoa ripoti ndogo juu ya kazi zake.
Habari zaidi juu ya Wafanyakazi hawa; Bi. Sayaka HOSOYAMADA alikuwa mwalimu wa hisabati katika Shule ya Sekondari ya Ngudu, Mwanza
Alifundisha hisabati kwenye O-level na A-level akilenga kuboresha utendaji wa wanafunzi na kuinua ari yao ya kusoma. Kwa kweli, wastani wa ufaulu katika mitihani ya shuleni hapo uliongezeka kutoka 9 mpaka 50 katika hiyo miaka miwili. Alijihusisha kwenye kazi za utawala wa shule na kuwasaidia walimu wengine shuleni.
Ms. Yumi KOYAMA alifanya kazi kwenye elimu ya mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mtwara. Aliendesha programu ya madarasa ya somo la mazingira kwenye shule za msingi, akiwa na kauli mbiu hii; “Kutunza mazingira yetu ni sawa na kutunza maisha yetu”. Katika programu hii, aliwafundisha wanafunzi kuhusu uhusiano kati ya mazingira na jamii, maji salama ni nini, na aina za takataka na jinsi ya kuzitupa. Anatumaini kwamba watoto waliofurahia kumsikiliza na kusoma juu ya mazingira wataleta mabadiliko, hata kama kidogo, kwenye maisha yetu ya baadaye Tanzania.
Ms. Noriko KOMATSU alikuwa muuguzi katika hospitali ya Wilaya ya Nachingwea, Lindi. Alitembelea mara kwa mara vituo vya afya vijijini Nachingwea, na kujaribu kuwafundisha akina mama njia nzuri ya kuwaangalia watoto wagonjwa. Alitambulisha kanuni ya 5S KAIZEN-TQM hospitalini, na kuchangia kwenye utunzaji na usafi wa sehemu za tiba kwa ajili ya hali nzuri ya wagonjwa hospitalini.
Ms. Norie SASAKI alifanya kazi ya elimu ya watoto wadogo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Alifanya kazi na walimu wa chekechea na kusisitiza umuhimu wa elimu ya watoto wadogo. Aliinua kitendo cha walimu kuchaza na watoto, hivyo kukuza ndani ya watoto hisia ya ubunifu na uvumbuzi.
Mr. Hayato WATANABE alikuwa mwalimu wa ufundi magari katika Chuo cha Ufundi Songea (VETA). Alilenga kuinua uasili na ubunifu wa wanafunzi. Baada ya miaka miwili ya kazi yake, mabadiliko kadhaa yalionekana katika wanafunzi na walimu. Kwa mfano ongezeko la uwezo wa ufundi katika kazi za vitendo na ujuzi wa ufundi magari ulionekana katika wanafunzi. Vilevile walimu wenzake waliongeza ujuzi wa ufundi magari, uangalifu juu ya usalama katika kazi za vitendo na uelewaji juu ya umuhimu wa kukarabati magari kabla ya kuharibika.

No comments:

Post a Comment