Sunday, June 5, 2011

TLS YAUNDA KAMATI YA WATU NANE KUSIMAMIA MCHAKATO WA UUNDWAJI KATIBA!

Chama cha Wanasheria Tanganyika ( TLS), kimeteua kamati ya katiba itakayosimamia mchakato wa uundwaji wa Katiba Mpya ikiwa ni pamoja na kuishauri Serikali kutoa nafasi kwa wananchi wote kushiriki katika mchakato huo. Akizungumzia kamati hiyo, Jijini Dar es salaam, Rais Chama hicho, FRANCIS STOLLA, amesema kamati hiyo itaundwa na wajumbe nane watakaoandaa rasimu ya katiba itakayotumika kuunda Katiba Mpya baada ya kusanya maoni kutoka kwa wananchi.
Aidha kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), MARIA KASHONDA, amekitaka Chama hicho kiandike upya Katiba ilioyopo kwa lugha nyepesi ili kila mwananchi aelewe kwa kina, kabla ya kusambaza katiba hiyo kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment