Wednesday, June 8, 2011

SERIKALI KUFANYA SENSA YA WATUMISHI WOTE WA SERIKALI NA TAASISI ZAKE KUDHIBITI MISHAHARA HEWA!

Serikali imepanga kufanya sensa ya watumishi wote wa serikali na taasisi zake kwa kuandaa siku maalum ya kuwalipa wafanyakazi wote dirishani ili kuthibiti mishahara hewa.
Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012, Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkullo amesema Wakuu wa Idara watawajibika kwa kuhakikisha kwamba wafanya kazi wanaolipwa ni halali.
MKULLO amesema kwamba watendaji wote wa Halmashauri na taasisi za serikali watawajibika ikibainika kwamba serikali imelipa mshahara kwa wafanyakazi hewa.

No comments:

Post a Comment