Thursday, June 9, 2011

TUNAWAJALI GROUP KUDHIBITI MADEREVA MATAPELI!

Mwenyekiti wa Taifa wa TUNAWAJALI GROUP Bw. ABEID CHEMBE (Kulia).
Chama cha Madereva Taksi nchini (TUNAWAJALI GROUP) kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kimepanga kutoa mafunzo ya polisi jamii watakaokuwa wakishughulikia matatizo mbalimbali ikiwemo kubaini madereva wanaofanya vitendo viovu kwa abiria.

Mwenyekiti wa Taifa wa TUNAWAJALI GROUP Bw. ABEID CHEMBE amesema mfumo huo pia utasaidia kulinda haki za madereva taksi nchini pamoja na kudhibiti matapeli ambao hawakidhi viwango vya kusafirisha abiria nchini.

No comments:

Post a Comment