Wednesday, June 8, 2011

KATIBA YABAINISHWA TENA BUNGENI LEO.....SERIKALI YASEMA HAIJAWAHI KUUNDA BARAZA LA USULUHISHI WA MGOGORO SERIKALI YA MUUNGANO!

                                                     Waziri SAMIA SULUHU (Kushoto). 
Serikali imesema haijawahi kuunda Baraza la Usuluhishi wa mgogoro kati ya Serikali ya Zanzibar na ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa hakuna mgogoro au mzozo wowote kuhusiana na ugawanyaji wa mapato ya muungano.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Musoma Vijijini CCM NIMROD MKONO, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano SAMIA SULUHU amesema serikali imeona hakuna umuhimu wa kuunda baraza hilo kwa sasa kwa kuwa kilichopo ni changamoto zinazotokana na Muungano ambapo mgogoro unapojitokeza usuluhishwa na tume ya pamoja ya fedha.
Katika swali lake Mbunge NIMROD MKONO alihoji kama kumejitokeza mgogoro wa mgawanyo wa mapato ya fedha za Muungano kwa nini Baraza la usuluhishi lisitumike kumaliza kero hiyo kama ilivyoanishwa kwenye Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment