Thursday, June 23, 2011

OUT KUWA MWENYEJI WA KONGAMANO LA KIMATAIFA KUJADILI UMUHIMU WA ELIMU HURIA!

                                                            Profesa TOLLY MBWETTE
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania, Profesa TOLLY MBWETTE, amebainisha kuwa Chuo hicho kimeteuliwa kuwa mwenyeji wa kongamano la Kimataifa linalotarajiwa kuanza Julai 12 mwaka huu, huku lengo likiwa ni kujadili umuhimu wa elimu huria katika maendeleo ya nchi za Ki-Afrika.

Profesa MBWETTE, amesema kongamano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri kutoka ndani na nje ya nchi huku mada mbalimbali zikitazamiwa kuwasilishwa na Wasomaji wa Kimataifa.
Ameongeza kuwa kongamano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 300 kutoka mataifa mbalimbali Barani Afrika huku likiwa limebeba kauli mbiu ya Njia ya kuweza kuziba pengo la maendeleo Barani Afrika kwa kutumia elimu huria.

No comments:

Post a Comment