Tuesday, June 14, 2011

NEC KUMTAFUTA MCHAWI KUTOKANA NA WAPIGA KURA WACHACHE 2010!

Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini (NEC), inatarajia kufanya utafiti wa kina kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini kufuatia kujitokeza kwa idadi ndogo ya wapiga kura katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka uliopita huku ikiahidi kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wadau hao juu ya uboreshaji wa chaguzi zinazokuja.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, RAJABU KIRAVU, amesema miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na Wadau hao ni pamoja na uboreshwaji wa Vifaa mbalimbali vinavyotumika katika uchaguzi na kuangaliwa upya kwa sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, LEWIS MAKAME, amesema uchaguzi uliopita ulifanyika kwa kuzingatia maadili ya uchaguzi ambayo yaliridhiwa na vyama vya siasa nchini.

No comments:

Post a Comment