Thursday, June 30, 2011

NAPE ATEMBELEA MAGAZETI YA MWANANCHI NA GLOBAL PUBLISHERS!

Katibu wa NEC, Itikati na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akizungumza na Wahariri wa magazeti ya Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, alipofaya ziara katika ofisi za kampuni hiyo, Tabata Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda na Kshoto ni Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Theophil Makunga, Mhariri Mrendaji gazeti la Mwananchi Dennis Msacky, na Mhariri wa Mwanaspoti Frank Sanga.

Meneja uzalishaji katika mtambo wa uchapaji magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Sameer Aher akimweleza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye sehemu ya mtambo huo inavyofanya kazi.Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa MCL Theophil Makunga.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Kiu, Ijumaa na Champion, Abdallah Mrisho, baada ya kuwasili Ofisi za kampuni hiyo,Mwenge, Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mhariri Kiongozi wa kampuni hiyo Oscar na Mhariri Kiongozi Oscar Ndauka na Mwandishi wa kampuni hiyo Luqman Maloto na wa pili kushoto ni Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda.
Nape akiwa katika ofisi za Global Publishers. Kushoto ni Abdallah Mrisho Wengine kutoka kulia ni, Sixtus Mapunda, Maloto, Ndauka na Mhariri kiongozi wa michezo wa Global Saleh Ally

No comments:

Post a Comment