Monday, June 13, 2011

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA UN KUHUSU UKIMWI!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Ukumbi wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York jana Juni 10, 2011, kwa ajili ya kuhudhuria hatua ya ufungaji wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi, uliozishirikisha nchi zaidi ya 30.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kulia), mkewe Mama Zakhia Bilal (wa tatu kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro (wa nne kulia) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim (wa pili kulia) na mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lediana Mng’ong’o (kulia). Kutoka (kushoto) ni Balozi wa Tanzania wa Umoja wa Mataifa, Ombeni Sefue, Naibu Waziri wa Afya , Sawere Nkya, Waziri wa Afya wa SMZ, Juma Duni Haji na Waziri katika Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais SMZ, Fatma Fereji, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo baina ya Makamu wa Rais na Naibu Katibu Mkuu jana Juni 10, 2011, New York. Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dkt. Asha Rose Migiro, wakati katibu huyo alipomtembelea hotelini kwake jijini New York, Juni 10, 2011 na kufanya naye mazungumzo.

No comments:

Post a Comment