Thursday, June 30, 2011

ASASI YA TWAWEZA KUZINDUA RIPOTI MPYA KUHUSU ELIMU KWA WATOTO!

Asasi huru ya Afrika Mashariki TWAWEZA ikishirikiana na taasisi ya UWEZO jumatatu ijayo watazindua ripoti mpya kuhusu Elimu kwa watoto ambapo lengo ni kutoa matokeo ya utafiti uliofanywa katika nchi za Afrika mashariki juu ya mfumo wa elimu nchini na namna unavyowaandaa watoto kupambana na changamoto zilizopo.

Afisa habari kutoka katika taasisi ya TWAWEZA,MKAMA MWIJARUBI amesema mambo makubwa yaliyozingatiwa katika ripoti hiyo ni kulinganisha kiwango cha watoto wenye umri kati ya miaka 5 hadi 16 ambapo ripoti imeangalia ulinganifu wa uwezo wa watoto kusoma na kufanya hisabati katika lugha kuu ikiwemo Kiswahili na Kiingereza.

No comments:

Post a Comment